UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ?
MAKALA
hii nimeiandika maalumu kwa watanzania na
wadau wangu wote , wanafunzi wa SHULE ZA MSINGI ,
SEKONDARI, na VYUO wanaopenda kujifunza
LUGHA YA KIINGEREZA AU KISWAHILI na lugha nyingne
ngeni lengo ni kuweza KUANDIKA na
KUONGEA kwa UFASAHA na UMAHIRI.
Limekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania wengi na
wanafunzi wetu kuanzia ELIMU AWALI, MSINGI,SEKONDARI , VYUO kutoweza
kuongea KIINGEREZA kwa ufasaha na
umahiri.Hata Lugha ya KISWAHILI ingawa
ni lugha yetu ya taifa bado ni
tatizo kwa watanzania wengi na wanafunzi kuongea
kwa ufasaha na umahiri ! TATIZO NI NINI ?
UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ? Kujifunza
LUGHA yoyote ni suala ENDELEVU {long
and permanent term } na siyo suala la
KUJIFUNZA LUGHA KWA WIKI TATU TU, AU
MIEZI MITATU TU ,AU MIEZI SITA
TU ! KAMA MATANGAZO YA BIASHARA YANAVYOJITANGAZA
. “ JIFUNZE LUGHA YA KIINGEREZA KWA
WIKI TATU “ hii si kweli ndugu
yangu.
LUGHA ni mtaji , inaweza kukufanikisha mambo
yako katika maisha ! Ndugu yangu MTANZANIA
kama wewe ni mbumbumbu wa Lugha
ya KISWAHILI au KIINGEREZA utachina
au utakwama katika masuala yako
yanayohitaji UMAHIRI katika lugha hizo
mbili . Kuna umuhimu sana kwa
ndugu yangu MTANZANIA kuwa MAHIRI katika
kutumia KISWAHILI au KIINGEREZA kwa ufasaha
na umahiri .
SIRI ZA
KUIKUZA LUGHA YA KIINGEREZA
---Huwezi
kuimiliki lugha yoyote kama huitumii.Mtu anaweza
kujidai kuwa kwa vile ni mswahili
na amezaliwa katika lugha hii
basi anaijua lugha. Hii si kweli
kabisa ndugu yangu .Kama ingekuwa hivyo
basi wote tungeweza kutumia na
kuielewa MISAMIATI na MISEMO yote
ambayo iko katika lugha yako.Kwanini basi
wengine wakiitumia MISEMO na
MISAMIATI hito wewe unatoka kappa , ni
kwa sababu huitumii.Kwa hiyo jambo la
msingi ni kuhakikisha kuwa unaitumia
lugha.
----Kwa
wale wanaojifunza lugha ya kigeni , jambo
la msingi ni
kuhakikisha kuwa unaitumia ili uweze kupata
uzoefu na hatimaye kuitumia kadri
unavyotaka.
-----KUITUMIA LUGHA MAANA
YAKE NINI ?
Izungumze au itumie katika MAANDISHI ; kama
ni lugha ngeni kwako.Kadri unavyoendelea
kuitumia katika mazungumzo au katika
kuiandika basi unakuwa na uwezo wa
kuielewa na utahitajika kupata
misamiati mipya.
----Hudhuria
katika mikutano na uhakikishe unatafuta
nafasi ya kuzungumza. Unapozungumza katika
matukio kama hayo maana yake
utapaswa kuchagua MANENO/ MISAMIATI na
kuyapanga ili uonekane unajieleza kwa
ufasaha na kile kinachokusudiwa. UWEZO
WA LUGHA UTAHITAJIKA.
-----Makongamano
, au hata ubishi wa kawaida mitaani
ni nafasi nzuri kwako wewe kuitumia
ili uweze kukuza uwezo wako wa
lugha. Na wewe uingie katika ubishi
halafu uangalie , fanya tathmini , baadaye , kwa
nini ulishindwa au kushinda, kwa nguvu
ya hoja au kwa hoja ya
nguvu.Kama unamiliki lugha unaweza
KUSHINDA kila KONGAMANO.
-----Jifunze
kutunga HADITHI au kuzisoma , KUTUNGA
MASHAIRI.Haya ni mambo pekee yanayoweza
kukufanya uhitaji uwezo mkubwa wa
lugha na hazina kubwa ya MISAMIATI.
UTATUNGAJE MASHAIRI KAMA
MISAMIATI YAKO NI MICHACHE ?
Aidha
ukitunga MASHAIRI au HADITHI utajikuta
nyakati zote unatafuta KAMUSI au
VITABU vya MISEMO na lugha
ili uweze kupata MANENO yanayofaa
katika utunzi wako kwa ajili hii
LUGHA yako inakua kwa haraka sana.
Lakini zuri sana hapa ni kuwa
kadri unavyoendelea kujihusisha na
utunzi wa MASHAIRI au HADITHI UNATUMIA
MUDA MWINGI KUFIKIRI , na jinsi
unavyoendelea kushughulika na mambo hayo,
uwezo wako wa KUFIKIRI NA KUTAFAKARI nao
huongezeka. Ongezeko la uwezo wako wa
KUFIKIRI ni matokeo ya kuwa na
UWEZO MKUBWA WA LUGHA.
----SIKILIZA
, Wengine hudhani KUSIKILIZA sio sehemu
ya kutumia / kujifunza LUGHA.
-----FUNGULIA
REDIO, utasikiliza MISEMO na MISAMIATI mbalimbali
ambayo utahitajika kuielewa ili
uweze kufuatilia kinachoelezwa .Kwa
hiyo basi kadri unvyoendelea
kuisikiliza ndivyo unavyoweza kuielewa
vizuri zaidi. Kwanza unapoisikiliza lugha ikizungumza
na wenyewe , kwa mfano , unajifunza
MATAMSHI SAHIHI , unajifunza MISEMO ambayo
huwezi kuipata katika matukio
mengine.
Unatakiwa kuwa mwangalifu katika kuchagua
vipindi , kama unachagua redio au televisheni ;
kuna TAARIFA YA HABARI ambayo , hutumia
LUGHA RASMI ili uweze KUJIFUNZA
MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA REJISTA
MBALIMBALI ZA LUGHA. Lakini chagua
vipindi vya DRAMA , yaani
MICHEZO YA KUIGIZA. Utajifunza LUGHA ikizungumzwa
katika mazingira yake halisi--- NATURAL
SETTING. Matamshi , mwitiko na uteuzi wa lugha
unaondana na mazingira.SIKILIZA VIPINDI
VYA DINI , SHULE , SAYANSI , UCHAMBUZI na kadhalika
ili uweze kupata MISAMIATI MBALIMBALI
KWA AJILI YA KUKUSAIDIA.
HITIMISHO
----Kama
unajifunza LUGHA YA KIGENI , fanya marudio , mazoezi
mengi na soma vitabu vingi vya hadithi
vya lugha hiyo.
-----Soma
ukiwa na KAMUSI na tafuta maana
ya neno usilolijua.
----Jizoeze
KUSIKILIZA na KUONGEA ukiwaiga wajuao ujifunzapo
lugha ya kigeni.
-----Sikiliza
MIHADHARA na REDIO ili ujifunze
kwa wengine wanavyotamka maneno.
-------Jikumbushe
MANENO magumu kila siku.
------Kila
nafasi unayoipata itumie kwa
kusoma.
------Pambana
na SARUFI za LUGHA YA KIGENI
kikamilifu.
------Jifunze
lugha ya kigeni kwa kuongea mara
kwa mara.
Asante
sana wadau wangu hasa WANAFUNZI wangu
kwa kusoma makala hii nzuri sana
kama utaweza mwonyeshe mwenzako naye
asome apate kuelewa jinsi
ya kukuza lugha ya kiingereza na
lugha nyingine.
No comments:
Post a Comment